FEAST OF CORPUS CHRISTI ANNOUNCEMENT (04/06/2023)

 

  1. We thank the good Lord for our work and business. On this First Sunday of the month, we invite those who have their Tithe, and those who paid directly to the Bank and Pay bill, we also invite parishioners who have redeemed their pledges this month to come forward for prayers and blessings. The Church Pay bill Number is 4042525 Account tithe
  2. We would like to thank our Jumuiya members and Parishioners who have already returned their tetra packs with their Lenten Campaign contributions. We urge all the Jumuiya Chairpersons to ensure that the remaining tetra packs are submitted through their respective Jumuiya treasurers to the CJPD desk after Mass. Those who did not get tetra packs can still make their contributions through our Church Pay bill 4042525, Account No: “LENTEN”
  3. The YOUNG CHRISTIAN WORKERS (YCW) is a transitional group between the Youth and Catholic Women Association and the Catholic Men Association. The devotional group cordially invites all parishioners of age 25-40 to join the group. Renewal and registration of new members will be taking place after mass. For more information regarding the group, there are representatives of the group outside the church to assist you with all enquiries.
  4. Doctors from Equity Afia Kitengela Branch have visited our parish today to offer free medical camp, we are encouraged to pass by their tent for body check-ups and medical advice.
  5. The PMC registration is ongoing, all the parishioners are requested to register all children ages 3yrs to 13yrs. Registration fee is 100/= per child. Registration is ongoing outside the PMC classes Note: Parishioners with children below 3yrs are requested NOT to leave the children in PMC class unattended.
  1. Infant baptism registration is ongoing and parents are requested to register through their Jumuiyas.
  2. Senior youth from Cathedral Ngong have visited our youths today

Jumuiya service

1st Mass: St. Raphael                           1st Mass: St. Rita

2nd Mass: Senior youth                         2nd Mass: Timothy

 

Matangazo ya 4/06/2023

MATANGAZO: 04/06/2023

  1. Leo ni Jumapili ya fungu la kumi,kwa wakristo ambao wamejitayarisha na pia wale ambao wametuma fungu lao kwa paybill ya kanisa na pia wakristu ambao wamelipa ahadi zao mwezi huu tunawaalika wajongee mbele kwa maombi na Baraka.Tunapokuja mbele tunaombwa kuweka nia zetu pamoja na fungu la kumi tunalomtolea Mungu.Paybill ya kanisa ni 4042525 account
  2. Tunawashukuru kwa dati wakristu wote ambao wamerudisha tetrapacks zao pamoja na mchango wao wa kampeni ya kwaresma.Wenyekiti wa Jumuiya zote wanaomba wahakikishe kwamba tetrapacks ambazo bado zimebaki zimerudishwa kwa meza ya CJPD pale nje baada ya misa hii kupitia kwa mweka hazina wa Jumuiya.
  3. The YOUNG CHRISTIAN WORKERS (YCW) ni kikundi cha mpito kati ya Jumuiya ya Vijana na Wanawake Wakatoliki na Jumuiya ya Wanaume Wakatoliki. Kikundi hiki kinawaalika waumini wote walio kati ya miaka 25-40 kujiunga na kikundi.

Usajili wa wanachama wapya utafanyika baada ya misa hii. Kwa habari zaidi kuhusu kikundi, kuna wawakilishi wa kikundi nje ya kanisa kukusaidia kwa maswali yote.

  1. Waunguzi kutoka Equity Afia wametembelea Parokia yetu leo kutoa huduma za afya kwa wakristu wote.Tunaombwa tupitie kwenye hema yao pale nje kwa ajili ya kupata huduma za afya ya mwili
  2. Usajili wa PMC unaendelea wazazi/walezi wanaombwa kusajili watoto wao walio kati ya miaka tatu na kumi na tatu (3-13yrs) kwa shilingi 100/= Kule kwa njengo la Sunday school.

Wazazi na walezi walio na watoto chini ya miaka tatu wanaobwa wasiwache watoto hawa peke yao kwa Sunday school.

  1. Usajili wa ubatizo wa watoto wachanga umeanza,wazazi wanaombwa kuandikisha watoto wao kupitia kwa Jumuiya.
  2. Vijana kutoka Cathedral Ngong wametembelea Vijana wetu leo.

 

Jumuiya service

1st Mass: St. Raphael                        1st Mass: St. Rita

2nd Mass: Senior youth                    2nd Mass: Tomothy

Matangazo ya Siku Kuu ya Pentekoste,28/05/2023.

MATANGAZO – PENTECOST SUNDAY 28/5/2023

1.Wakristo ambao waliacha kupokea  na hawako kwa ndoa na wangetaka kuanza kupokea Sakramenti Takatifu, wanaombwa kuona Padre kwa ofisi siku na masaa ya kazi au, wapinge simu kujadiliana na Padre siku ingine yeyote wanaweza kupatikana.

2.Jumamosi ijayo (3/6/2023) ikiwa ni Jumamosi ya kwanza ya mwezi, ni siku ya maombi(recollection) kuanzia saa tatu asubuhi (9.00am) hadi saa sita mchana (12:00 noon). Hakutakuwa Misa ya asubuhi kama ilivyo kawaida.

3.Alhamisi tarehe moja June (1st June) ambayo Wakenya watasherehekea  Madaraka day, Misa itaanza saa tatu asubuhi (09.00am).

4.Jumapili ijayo tarehe nne June (4th June) vijana kutoka Ngong Cathedral Plan watatembelea kanisa yetu ili wawe na kikao maalum pamoja na vijana wetu. Vijana wote wanahimizwa kuhudhuria siku hiyo.

5.Kikundi cha Josil Ushindi (Singles Church Support) wanakubushwa mkutano wao baada ya hii Misa. Wakristo ambao ni single na wangetaka kujiunga na kikundi hiki wamekaribishwa.

6.Jumapili ijayo tarehe 4/6/2023 wahudumu kutoka hospitali ya Equity Afia, watatembelea kanisa letu kupeana vipimo tofauti tofauti kwa bei nafuu. Wakristo wanaombwa kuchukua fursa hii kujua hali ya afya yao.

7.Jumuiya service

1st Mass: St. Joseph the Worker                              1st Mass: St. Raphael

2nd Mass: St. Padre Pio                                               2nd Mass: Senior Youth

 

8. Matangazo ya PFC

ANNOUNCEMENT ON 28TH MAY 2023 ON THE DAY OF PENTECOST

ANNOUNCEMENTS: PENTECOST SUNDAY 28/5/2023

  • We have begun a registration for parishioners who would like to be readmitted into the Holy Sacrament of Eucharist. Those interest are requested to come and meet the Priest during office hours or make an appointment with him.
  • This coming Saturday (3/06/2023), being the first Saturday of the month there will be a parish recollection from 9am. All parishioners are welcome. There will be no morning mass that day.
  • Thursday 1st of June, will be a public holiday and Mass will be at 9am.
  • Next Sunday 4th June, the senior youth from Ngong Cathedral Plan will visit our church for an exchange programme with our youths. All the youth of our church are encouraged to be present on that day.
  • Josil Ushindi (Singles Church Support) Group will have a meeting today after second Mass at the balcony. New members are invited to join.
  • Next Sunday 4th June, Equity Afya- Kitengela branch will be offering a free medical camp for our Parishioners – Christians are encouraged take advantage of this opportunity to do body checkups.

 

Jumuiya service

1st Mass: St. Joseph the Worker                1st Mass: St. Raphael

2nd Mass: St. Padre Pio                                            2nd Mass: Senior Youth

 

PFC announcements

 

 

 

MATANGAZO 23RD MAY 2023

7TH SUNDAY OF EASTER: ANNOUNCEMENTS 20/05/2023

  1. This Sunday is World Communication Day. We thank God Our Father for letting us know continuously about his love and care for us and our Salvation in Jesus Christ and the Holy Spirit. On this World Day of Communication, we are reminded of our duty to support the diocesan projects for communication. We kindly request for a second collection for our diocese.
  2. On Saturday 27th May we will have the Opus Dei monthly Day of Recollection for ladies and gentlemen. The ladies begin at 8.00 am with the Sacraments of Reconciliation/ Confessions. The gentleman session will start at 2.00 pm. All are welcome.
  3. The Parish Senior Youth group will visit Sidon children’s home in Roysambu on the Saturday of the 27th May 2023 All youth are called upon to participate. They are also seeking our help and support in funding, foodstuffs clothing and prayer. All help is highly appreciated.
  4. The Commissioning of all church and group leaders will take place on Sunday 28th. Those to be commissioned are reminded to be present, dressed for the occasion, and bring with them their Bible and Holy Rosary and other required items.
  5. Today after 1st Mass, the Catholic Men Association will hold their training and seminar in the new building. All CMA members are invited.
  6. On 4th June, the senior youth from Ngong Cathedral will visit our church for an exchange programme with our youths. All the youth of our church are encouraged to be present on that day. Today they will also have a talk on mental health after Second Mass, they are all encouraged to remain behind.
  7. Josil Ushindi (Singles Church Support) Group are invited to their meeting coming Sunday 28th May 2023. New members are invited to join.
  8. We would like to thank our Jumuiya members and Parishioners who have already returned their tetra packs with their Lenten Campaign contributions. We urge all the Jumuiya Chairpersons to ensure that the remaining tetra packs are submitted through their respective Jumuiya treasurers to the CJPD desk after Mass. We urge everyone to ensure that these are received by 28th May. Those who did not get tetra packs can still make their contributions through our Church Paybill 4042525, Account No: “LENTEN”

 

**Invite CJPD Chair to give a brief overview on Lenten Campaign contributions.

 

**Invite the Parish Chair to introduce Church Communication Team.

Jumuiya service

Today                                                Next Sunday

1st Mass: St. Mary                          1st Mass: St. Joseph the Worker

         2nd Mass: St. Peter and Paul           2nd Mass: St. Padre Pio

 

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU KWA SIKU ZOTE TISA

*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU KWA SIKU ZOTE TISA
*BAADHI YA NYIMBO KWA ROHO MTAKATIFU*

*NJOO WANGU MFARIJI*
*Njoo wangu Mfariji, Yako shusha mapaji, Roho Mungu njoo*
1. Hekima nishushie, Mungu nimfuatie, Roho Mungu njoo
2. Akili nijalie, imani nizidie, Roho Mungu njoo
3. Nieneze shauri, imani nizidie, Roho Mungu njoo
4. Nizidishie nguvu, nsifanye ulegevu, Roho Mungu njoo
5. Elimu nieleze, hakika niongoze, Roho Mungu njoo
6. Ibada niwashie, Peke nikupupie, Roho Mungu njoo
7. Uchaji nitilie, dhambi nizichukie, Roho Mungu njoo.

*NJOO ROHO MTAKATIFU*
*Njoo Roho Mtakatifu, shusha mapaji (kweli) niwe imara x2*
*Leta nuru ya mwanga wako, ifikie moyoni mwangu x2*
1. Roho mwenye hekima, Roho wa shauri na nguvu.
2. Nipatie elimu nitambue nafsi yako.
3. Nipatie ibada nikusifu daima milele.
4. Roho mwenye uchaji washa moto wako wa mapendo.

*UJE ROHO (SEKWENSIA)*
1. Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu, roho zetu kwa mwangao
2. Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji, uje mwanga wa mioyo
3. Ee Mfariji mwema sana, ee Rafiki Mwanana, ewe raha mustarehe
4. Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto burudisho, u mfutaji wa machozi
5. Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waumini, neema yako mioyoni
6. Bila nguvu yako Wewe, mwanadamu hana kitu, kwake yote yana kosa.
7. Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu, na kuponya majeraha
8. Ulegeze ukaidi, pasha moto ubaridi, nyosha upotovu wote
9. Wape waamini wako, wenye tumaini kwako, paji zako zote saba.
10. Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila, wape heri ya milele.
11. Amina aleluya, amina aleluya, amina aleluya.

*NJOO ROHO MTAKATIFU*
1. Njoo Roho Mtakatifu, angalia zetu nyoyo, waletee neema nguvu, wakosefu viumbevyo.
2. Majina yako Mfariji, shina la uzima pendo, wake Mwenyezi upaji, mafuta ya roho moto.
3. Ndiwe mnye mapaji saba, wa Mungu kuume mkono, mshika uhadi wa Baba, mtoa kwa ndimi maneno.
4. Angalo litung’arie, moyo kwa pendo tushushe, nguvu neema tujalie, wanyonge wasabilitishe.
5. Shetani mbali mkimbize, amani utupatie, tukufuate tuongoze, maovu utukingie
6. Baba Mungu tujulishe, pia Mwana tumkubali, Roho tukuungamie, mtokea wao wawili.

*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA KWANZA*
*IJUMAA : ROHO MTAKATIFU ANATUFARIJI*
Yesu alipokuwa akiagana na mitume wake, kabla ya kupaa mbinguni, aliwaambia wasiondoke Yerusalemu mpaka hapo watakapokuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Aliwaambia: “Wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni, mtajazwa nguvu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yuda na Samaria, hata kwenye mipaka yote ya dunia.” (Mdo.1:8)
Waliendelea kusali pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni mpaka siku ya Pentekoste. Waliomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze na mapaji yake. Na baada ya siku tisa Roho Mtakatifu aliwashukia hao kundi dogo nao wakawa chanzo cha Kanisa lililopata kuenea duniani kote.
Siku hizo tisa za kusali zinaitwa NOVENA; na kila mwaka wakati huu, wakristu wakifuata mfano wa mitume, wanasali muda wa siku tisa kabla ya Sikukuu ya Pentekoste. Wanamuomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze nguvu na wingi wa mapaji yake.
Wakati huu wa NOVENA , Tunayo mengi ya kuliombea Kanisa na kujiombea sisi wenyewe. Kwa hiyo tumuombe Roho Mtakatifu atusaidie kusali vema na kuomba yale yote tunayohitaji kwa maslahi yetu ya roho na mwili.
Na kama mtume Paulo alivyowaambia wale waKristu wa kwanza, Roho Mtakatifu huja kutufatiji katika udhaifu wetu. Basi tumuombe atufariji kwa sala hizi za NOVENA, Atuwezeshe kusali na kuomba inavyotupasa kusali.
1) Ee Baba wa milele, tunakuomba umtume Roho Mtakatifu atushukie sisi taifa lako awashe ndani yetu moto wa upendo wako.
*W. Twakuomba utusikie.*

2) Ee Baba mwema, tunakuomba utujalie faraja ya Roho Mtakatifu sisi wana tulio katika dhiki na taabu nyingi mno hapa duniani. *W.* *Twakuomba utusikie.*

3) Ulijalie Kanisa lako mapaji ya Roho wako Mtakatifu, liweze kutekeleza vema utume wake wa kuhudumia watu wote hapa duniani.
*W. Twakuomba utusikie.*

4) Utujalie sisi kudumu katika NOVENA hii mpaka mwisho kama Maria na mitume walivyodumu pamoja wakisali kabla ya Pentekoste ile ya kwanza.
*W. Twakuomba utusikie.*

5) Utujalie neema zote zinazohitajika ili tuweze kumshuhudia Kristu popote kwa mwenendo na matendo yetu ya kila siku, tukiongozwa na Roho Mtakatifu.
*W. Twakuomba utusikie.*
6) Uzijalie familia zote za wakristu neema na nguvu za Roho Mtakatifu tupate kuendelea pasipo kuchoka katika sala na katika matendo mema siku zote.
*W. Twakuomba utusikie*

7) Ewe Roho Mtakatifu, uwajalie vijana wetu moyo wa ujasiri, wapate kulijenga kanisa lako na kueneza utawala wako katika jumuia zetu za Kikristu.
*W. Twakuomba utusikie.*

*TUOMBE;*
Ee Mungu, uliye muumba wa vitu vyote , tunakuomba utusikilize kwa wema sala zetu sisi taifa lako, utuongoze sote tufuate siku zote utaratibu wa mapenzi yako; naye Roho Mtakatifu atutegemeze mpaka mwisho wa novena hii. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu .
*W. Amina.*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)*
*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA PILI*
*JUMAMOSI : ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUENEZA INJILI*
“Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika utawala wa Mungu,”
(Yn. 3:5).
Kanisa limepewa na Yesu ujumbe wa kuwaletea watu wote uzima mpya, uzima wa Mungu. Yesu aliwaambia mitume wake: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi mkawafanye watu wa makabila yote kuwa wafuasi wangu. Wabatizeni kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kuyashika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote mpaka mwisho wa nyakati (Mt.28:18-20).
Sisi tuliobatizwa tumepata kuwa viungo vilivyo hai vya Mwili wa Fumbo wa Kristu; kwa Kipaimara tumeimarishwa na kuthibitishwa na Roho Mtakatifu. Tumekuwa taifa teule. Tumeshirikishwa ule ukuhani wa Kristu. Tumepokea ujumbe wa kueneza utawala wa Mungu.
Tunapopokea Sakramenti, na hasa ile Sakmenti ya Ekaristi, tunalisha imani na kuongeza mapendo, ambayo ni msingi wa utume wowote ule. Mapendo yanatuhimiza kueneza utawala wa Mungu na kumpenda Yesu Kristu aliyekuja kuwakomboa wanadamu wote.
Kila aliyebatizwa anao wajibu wa kueneza imani ya Mungu na utawala wake. Kwa hiyo tumuombe Roho Mtakatifu atuwezeshe kutimiza wito huo.
1) Ee Baba wa mbinguni tunakuomba umpeleke Roho Mtakatifu aliangaze kanisa na kuliongoza, liweze kuwafikishia mataifa yote habari njema ya wokovu.
*W. Twakuomba utusikie*
2) Ee Yesu Mkombozi wetu, umtume Roho Mtakatifu awahimize wakristu wapate kutimiza wajibu wao wa kueneza neno lako popote duniani
*W. Twakuomba utusikie*

3) Ewe Roho Mtakatifu Mfariji, uamshe katika mioyo ya vijana wengi hamu ya kupenda kulitumikia kanisa lako na kulihudumia taifa lako kwa uaminifu.
*W. Twakuomba utusikie*

4) Ewe mwanga wa mataifa , uwajalie wanafunzi wasikie sauti yako mioyoni mwao, nawe unapowaita wasikose kuisikia sauti yako, wawe tayari kujitoa kwa ajili ya ndugu zao.
*W. Twakuomba utusikie.*

5) Uwasaidie wazazi wawalee vema watoto wao; uwatie moyo katika wito wao, wapate pia kuishiriki vema ile kazi ya kueneza neno lako kwa jirani zao.
*W. Twakuomba utusikie*

6) Ewe Roho Mtakatifu, uwasaidie wakristu wote kueneza habari njema ya wokovu, kwa sala, kwa sadaka na kwa mifano ya maisha yao ya uchaji.
*W. Twakuomba utusikie*
7). Ewe mpaji wa mema, uwajalie waumini mapaji yako saba, wasichoke kulieneza neno lako kwa hekima pasipo hofu.
*W. Twakuomba utusikie.*
*TUOMBE*
Ee Mungu, unapenda watu wote waokoke, waifikie kweli yako. Tunakuomba uwapeleke wafanyakazi walio wengi na wema katika shamba lako. Uwajalie kulihubiri neno lako kwa imani kuu ili neno lako lienee na kupokewa na mataifa yote, wapate nao kukujua wewe peke yako Mungu wao, Mungu wa kweli. Tunaomba hayo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeliongoza kanisa lako sasa na milele.
*W. Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)*
*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TATU*
*JUMAPILI: ROHO MTAKATIFU ANATUFANYA KUWA MITUME*
Bwana alisema kwa kinywa cha nabii Yoeli; “Katika siku zile za mwisho asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, waume kwa wake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto….hata watumishi wenu watamiminiwa Roho wangu katika siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu. (Mdo.2:17-21)
Siku ile ya Pentekoste, bada ya Roho Mtakatifu kulishukia kanisa, mitume waliwakumbusha watu maneno haya ya nabii Yoeli, na miaka mingi baadae, Petro aliwaandikia barua Wakristu wa kwanza akawaambia; kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile wakili mwema wa zawadi mbali mbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu aliyojaliwa na Mungu ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristu, ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele (Pet 4;10-11).
Mtaguso wa Pili wa Vatikano ulitukumbusha jambo hilo hilo uliposema; “Roho Mtakatifu anayetakasa taifa la Mungu kwa njia ya Sakramenti amewapa waumini mapaji ya pekee na kumjalia kila mmoja kadiri apendavyo. Kwa hiyo kila mmoja amgawie mwenzake kadiri ya vipawa alivyopewa, awe mgawaji mwaminifu wa neema ya Mungu, alijenge kanisa zima katika upendo.
Tunao wajibu wa kutumia vipawa tulivyojaliwa na Roho Mtakatifu kwa manufaa ya kanisa zima, na kwa faida ya watu wote. Tuunganike sote pamoja na wachungaji wote katika kazi hiyo ya utume. Tumuombe basi Roho Mtakatifu atusaidie kutumia vema vipawa vyake alivyotujalia.
1) Ewe Roho Mtakatifu uwape wakristu neema na nguvu za kutumia vema vipaji ulivyowajalia kwa ajili ya kujenga kanisa lako popote duniani, kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
*W. Twakuomba utusikie*

2) Utujalie sisi sote mapaji yako saba, tupate kukutumikia kwa uchaji.
*W. Twakuomba utusikie*

3) Utujalie tuwe mitume wa kweli wa wenzetu, tushirikiane na wachungaji wetu katika huduma za kuwaongoza watu wote na kuwafikisha mbinguni.
*W. Twakuomba utusikie.*

4) Utujalie hekima na nguvu za kuwahudumia watu wote kwa mapendo ya kweli yasiyo na kinyume
*W. Twakuomba utusikie.*

5) Utujalie neema ya kumpenda Mungu kwa moyo wote na kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe.
*W. Twakuomba utusikie.*

6) Utupe neema ya kulisikia neno lako na kulifuata, nayo mawazo yetu na matendo yetu yafuate daima mwongozo wako mtakatifu
*W. Twakuomba utusikie*

7) Uwazidishie mapaji yako wale wote wanaotumia vyema vipawa vyao, uwarudishe na wale wanaotumia vibaya rehema zako.
*W. Twakuomba utusikie.*

*TUOMBE;*
Ewe Roho Mungu ndiwe uliyewapa waumini vipawa vyako kwa kadiri unavyotaka. Utujalie tuyapokee na kuyatumia vyema mapaji yako mengi kwa ajili ya utukufu wa Jina lako na kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
*W. Amina*
*Litania ya Roho Mtakatifu …. (soma hapo chini)*
*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NNE, *
*JUMATATU : ROHO MTAKATIFU ANALIUNGANISHA KANISA*
“Atakapokuja huyu Roho wa kweli , atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yn 16:13)
Baada ya kusema hayo, Yesu aliinua macho yake kuelekea mbinguni akasema “Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba Wewe ulinituma (Yn 17:4,21).
Nasi twamuomba Mungu Mwenyezi alijalie kanisa lake umoja wa kweli, awaunganishe wakristu wa madhehebu yote katika zizi moja chini ya mchungaji mmoja.
Popote duniani watu wengi, makundi kwa makundi wanavutwa na neema hiyo ya kuungana na kuufikia umoja wa Kanisa. Hata ndugu zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo wa Roho Mtakatifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja chini ya mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona kwamba kwa namna fulani wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kumshuhudia hata kwa kumwaga damu yao.
Tena katika hao ndugu zetu waliojitenga, Roho Mtakatifu analisha katika mioyo yao ile ya imani inayowaunganisha wafuasi wote wa Kristu. Tumwombe basi Mwenyezi Mungu atujalie hima huo umoja wa Kanisa lake tunaouania mno.
1) Ee Yesu Bwana wetu wewe umetuombea kwa Mungu Baba tuwe itu kimoja kama Wewe ulivyo kitu kimoja na Baba. Utujalie huo umoja, ili ulimwengu uone na kukiri kwamba ndiwe Bwana na Mkombozi wa watu wote
*W. Twakuomba utusikie.*

2) Ee Yesu utujalie moyo wa kulishika neno lako kwa uaminifu, wala usituache kufuata njia zetu sisi wenyewe na kufarakana.
*W. Twakuomba utusikie*

3) Ee Yesu uliye Mchungaji wetu mwema, ondoa ndani yetu ile tabia ya utengano, tupate kuwa sote kundi moja chini yako wewe uliye mchungaji wetu mmoja.
*W. Twakuomba utusikie*

4) Ee Yesu, uliye Mchungaji mkuu, uwajalie wachungaji wetu wawe siku zote na upendo wa Jina lako, wasichoke kulichunga vema kundi lako hapa duniani na kuliweka pamoja lisitengane.
*W. Twakuombaa utusikie*

5) Ewe Roho Mtakatifu, uziangaze akili za watu wote, wapende siku zote kuishi kwa amani, umoja na mapendano
*W. Twakuomba utusikie*

6) Ee Mungu, utufungulie …… wa muungano wako wa kweli sisi tulio ndugu katika Bwana wetu Yesu Kristu.
*W. Twakuomba utusikie*

7) Utujalie mapatano na amani, tudumu tumeungana katika familia zetu, katika jimbo letu na katika nchi yetu yote.
*W. Twakuomba utusikie.*

*TUOMBE;*
Ee Mungu, utuunganishe sisi kondoo wako tuliotawanyika, tuwe chini ya Mwanao mpenzi, tupate sote kuushiriki ule utawala wako wa kweli na haki, utawala wa neema na amani, utawala wa upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu
*W. Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU …. (soma hapo chini)*

*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TANO,*
*JUMANNE:ROHO MTAKATIFU ANAWATAKASA WAUMINI*
Walio wa Mungu watafuata yaliyo ya Mungu, na walio wa dunia hufuata yaliyo ya dunia,. Ni mauti kutosheka na mambo yaliyo ya dunia. Uzima na faraja ya kweli hupatikana tu katika mambo ya Mungu.
Kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi kutenda lolote jema. Kuweza kwetu kwatoka kwa Mungu, kwatoka kwa Yeye anayetupa kujua, kupenda na kutenda.
Mtu anapotenda dhambi, hawezi kuongoka ila kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ndiye anayempa mkosefu neema ya kutambua ubaya wa kosa lakena kuamua kuliacha. Ndiye anayempa pia mkosefu kutambua uzuri wa neema aliyoipoteza na kumrudishia neema hiyo. Ndiye anayempa nguvu za kuidumisha neema hiyo na kuiongeza.
Isitoshe, Roho Mtakatifu ndiye anayemuwezesha mtu kuwa na maendeleo katika fadhila na utakatifu. Ndiye anayemjalia imani iliyo msingi wa maisha ya kiKristu. Ndie anayetujalia akili ya kushika mafumbo ya dini yetu na kuishi imani yetu mpaka kufa.
Lakini imani peke yake haimtoshi mtu aokoke. Imani pasipo matendo haifai kitu; imani bila matendo imekufa (Yak 2:28) Roho Mtakatifu anamuwezesha mtu kumuamini Mungu na kumenda kuliko vitu vyote na kumpenda jirani kama kujipenda mwenyewe. Ndiyo maana Roho Mtakatifu huitwa chanzo cha matendo yetu yote yaliyo mema. Basi, tumuombe Roho Mtakatifu aitakase mioyo yetu sisi waumini wake, atuzidishie imani, atuwezeshe kutenda matendo yaliyojaa imani.
1) Ewe Roho Mtakatifu, utudumishie imani, uyatakase mawazo ya mioyo yetu yafuate daima maongozi yako na amri zako
*W. Twakuomba utusikie*

2) Uzigeuze nia zetu zipate kumuelekea daima Mungu
*W. Twakuomba utusikie*

3) Utuwezeshe kuelekea katika utakatifu na kutenda mema kwa imani siku zote za maisha yetu
*W. Twakuomba utusikie*
4) Utuzidishie imani matumaini na mapendo, tuweze kushika kwa moyo thabiti yale yote tunayofundishwa na kanisa lako takatifu
*W. Twakuomba utusikie*

5) Uiwashe mioyo yetu na moto wa mapendo yako, tupate kumpenda Mungu kweli na kumpenda jirani yetu pasipo unafiki.
*W. Twakuomba utusikie*

6) Utusaidie tuishi vema kwa imani na matumaini siku zote za maisha yetu.
*W. Twakuomba utusikie*
7) Utujalie kudumisha mioyoni mwetu ile neema ya utakaso tuliyoipata mwanzo katika ubatizo wetu.
*W. Twakuomba utusikie*

*TUOMBE;*
Ee Mungu, mbele yako mioyo yetu i wazi; wewe wayajua yote, wala hakuna siri iliyofichika mbele yako. Uyatakase mawazo ya mioyo yetu kwa kutupelekea Roho Mtakatifu, ili tuweze kukupenda na kukutukuza kama inavyostahili. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu
*W. Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)*
*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SITA*
*JUMATANO :ROHO MTAKATIFU ANATUPA NGUVU*
“Nitamuomba Baba , naye atawapelekea Mfariji mwingine atakaye kaa nanyi siku zote”. Katika maisha yenu hapa duniani tunahitaji mno kitulizo cha Mungu. Ni jambo la hekima kutafuta kitulizo hicho kwa Mungu wala si kwa viumbe; maana kitulizo kinachopatikana kwa viumbe hapa duniani hakidumu; bali kitulizo kitokacho kwa Mungu ni cha kudumu.
Roho Mtakatifu ndio kitulizo chetu cha kweli. Baba ndiye aliyetuumba, Mwana ndiye aliyetukomboa, Roho Mtakatifu ndiye aliyetutakasa mioyo yetu na kutufariji.
Kazi ya Roho Mtakatifu sio tu kuwatuliza wale walio na huzuni, bali pia kuwapa moyo wa kuvumilia taabu zozote kwa saburi.
Tunahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tuweze kuishi maisha mema ya kikristu. Katika juhudi zetu za kumtumikia Mungu mara nyingi tunakutana na shida; naye Roho Mtakatifu ndie anayetufariji kwa kutupa nguvu za kupambana na matatizo yote. Maisha yetu hapa duniani yamejaa misalaba. Na misalaba hiyo hatuwezi kuichukua kwa nguvu zetu wenyewe. Roho Mtakatifu ndie anayetupa nguvu za kuvumilia. Basi, tumuombe aje kutufariji na kutupa nguvu za kuchukua msalaba wetu kwa saburi kila siku.

1) Ee Yesu Bwana wetu, tunakusihi Wewe na Baba mumtume Roho Mtakatifu atufariji, awajalie kitulizo wale wote walio katika taabu na majonzi
*W. Twakuomba utusikie*

2) Ewe Roho Mtakatifu, uwafariji wale walio katika tabu za namna zozote ili waweze kuvumilia kwa saburi mateso yao kwa faida ya Roho zao na roho za ndugu zao.
*W. Twakuomba utusikie*

3) Uwafariji wale walio wagonjwa, uwajalie afya ya roho na ya mwili
*W. Twakuomba utusikie*

4) Uwasaidie yatima, wajane na wote walioachwa, wasikose kupata siku kwa siku mahitaji yao ya lazima
*W. Twakuomba utusikie*

5) Wajalie wale wote walio walegevu na wakosefu neema ya kuongoka na kurejea hima katika amani ya upendo wako
*W. Twakuomba utusikie*
6) Uwaimarishe wale walio wema, uwajalie neema ya kudumu wasilegee katika kutenda mema leo na kesho na siku zote za maisha yao.
*W. Twakuomba utusikie*

7) Utujalie nguvu za kutafuta na kudumisha amani ya kweli katika mioyo yetu na kati ya ndugu zetu katika jumuia zetu za kikristu
*W. Twakuomba utusikie*

*TUOMBE*
Ee Bwana Mungu wetu, tunakuomba neema ya Roho Mtakatifu ituangaze akili na mioyo yetu na kutujaza nguvu ya upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
*W. Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)*
*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SABA*
*ALHAMISI:ROHO MTAKATIFU ANATUPA HEKIMA*
Hekima tunayopewa na Roho Mtakatifu si sawa kama hekima inayopatikana katika ulimwengu huu.
Hekima ya Roho Mtakatifu ni ile Mtk. Paulo aliyowaambia Wakorintho ya kuwa; ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana kama wangaliielewa,hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu. Lakini, ni kama yasemavyo maandiko; mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao (1Kor 2;8-9).
Mtk. Paulo alisema kama vile roho ya mtu ndiyo yenye kufahamu na kutambua yaliyo ndani yake; hivyo pia Roho Mtakatifu ndiye anayefahamu mambo ya Mungu na kutufumbulia sisi mioyoni mwetu.
Katika Sikukuu hii ya Pentekoste tunatazamia kumpokea Roho Mtakatifu. Yeye aliye hekima ya Mungu atatufumbulia siri za Mungu na ukweli wake. Ndiye atakayeamsha ndani yetu mapendo ya Yesu Msulibiwa , Mkombozi wetu. Ni yeye atakayetuongoza kutenda mema na kuacha mabaya; tunahitaji sana Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku, tupate hekima ya kuchagua na kutenda daima yaliyo mema. Katika novena hii tuzidi kumuomba Mungu atushushie Roho Mtakatifu, atujaze na hekima yake.
1) Ee Mungu, uwabariki viongozi wa dini na wasaidizi wao, wapate kutuongoza kwa hekima na mapendo
*W. Twakuomba utusikie*

2) Ewe Roho Mtakatifu, utujalie hekima ya kutambua Mambo ya Mungu na kuyatekeleza kwa uchaji.
*W. Twakuomba utusikie*

3) Utujalie kuyajua mapenzi ya Mungu na kuyapokea kwa furaha *W. Twakuomba utusikie*

4) Uamshe ndani yetu mapendo ya Yesu msulubiwa , utuwezeshe kutimiza vema wajibu wetu kama wafuasi wa kweli wa Kristu Bwana wetu.
*W. Twakuomba utusikie*

5) Utuwezeshe kuchagua daima yaliyo mema na kuyatekeleza, tupate kulijenga na kulidumisha kanisa lako hapa duniani
*W. Twakuomba utusikie*

6) Utuepushe na mafundisho yoyote yaliyo na upotovu, utujalie hekima ya kuzidi kutambua ukweli wako na mafundisho yako yaletayo wokovu.
*W. Twakuomba utusikie*

7) Hekima ya Roho Mtakatifu ituongoze katika satfari ya maisha yetu hapa duniani, tupate mwishowe kukurudi Wewe Muumba wetu uliye mwanzo wetu na mwisho wetu.
*W. Twakuomba utusikie*

*TUOMBE;*
Ee Mungu, Baba wa utukufu, tunakuomba utupe Roho wako wa hekima, atuwezeshe kukufahamu vema, atuongoze kuishi maisha yenye kukupendeza. Utusaidie kupambana na matatizo ya maisha, tupate kuishi maisha mema hapa duniani na mwisho tupate tunzo la heri na furaha yako huko mbinguni. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
*W. Amina.*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)*

*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NANE*
* IJUMAA: ROHO MTAKATIFU ANATUPA MWANGA*.
Roho Mtakatifu anaangaza akili zetu tuweze kuona ukweli wa Mungu na kuufata. Bila Roho Mtakatifu akili zetu zimo katika giza nene, wala hatuwezi kuona njia ya kutuelekeza kwa Mungu.
Mungu alipoumba ulimwengu, dunia ilikuwa giza tupu, haina kitu. Mungu alisema; “Iwe nuru”, ikawa nuru, Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema (Mwa 1;3-4) vivyo hivyo akili ya binadamu bila nuru ya mwanga wa Roho Mtakatifu, ni tupu, ina giza, haiwezi kuona mambo yanayotuelekeza kwa Mungu. Tukiwa na nuru ya Roho Mtakatifu tunaona ukweli wa Mungu jinsi ulivyo.
Roho Mtakatifu anapoijia roho ya mtu, anaiangaza akili yake iweze kuona mambo yanayofaa kwa wokovu. Naye akiisha kuiangaza akili ya mtu huimarisha utashi wake na kumwezesha kuchagua daima yaliyo mema.
Roho Mtakatifu huiangaza akili iweze kuona ukweli. Kabla ya kuwaaga mitume, Yesu aliwaambia kuwa atawapelekea mfariji mwingine atakayekaa nao siku zote. Roho wa kweli ambaye dunia haiwezi kumpokea kwa sababu hawakumfahamu, lakini wao mitume watamfahamu kwa maana atakaa nao siku zote. Yesu ametuahidi pia sisi Roho huyo akae nasi
Leo hivi duniani kuna uwongo na udanganyifu mwingi; kuna dhuluma, vita, na maovu ya kila namna. Hii ni kwa sababu dunia haijamtambua bado Roho Mtakatifu na kumpokea Yeye aliye mwanga wa dunia na asili ya kweli yote.
Mtaguso wa Pili wa Vatikano watambua ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika kanisa na katika mioyo ya waumini kama katika hekalu. Roho Mtakatifu analiongoza kanisa na kulifanya liwe na umoja; analipamba na mapaji yake mabalimbali.
Tumuombe Mungu Baba ampeleke huyo Roho Mtakatifu katika kanisa lake, aliongoze na kulilinda lisipate kutengana, bali lisaidie kueneza utawala wa Mungu popote duniani.
1) Ewe Roho Mtakatifu, utujalie kuona mwanga wa kweli yako na kuifuata.
*W. Twakuomba utusikie*

2) Uwape waregevu neema ya kuirudia tena njia ya kweli yako.
*W. Twakuomba utusikie*

3) Utuwezeshe sisi sote waamini wako tutembee siku zote katika nuru ya kweli yako na sheria zako.
*W. Twakuomba utusikie*

4) Utuangazie akili ya mioyo yetu tuchague daima yale yanayakupendeza.
W. Twakuomba utusikie

5) Uwape mwanga wako viongozi wetu wa dini na serikali, wapate kutuongoza kwa hekima na uchaji, wasisahau kamwe kwamba uwezo walionao unatoka kwa Mungu.
*W. Twakuomba utusikie*

6) Utupe mwanga wako tuwaone watu wote kama ndugu zetu. Tuishi kindugu na kusaidiana kindugu.
*W. Twakuomba utusikie*
7) Ewe Roho Mtakatifu ndiwe mpatanishi wa mioyo,; tunakuomba uondoe udhalimu, uonevu, udanganyifu na maovu yote katika mioyo ya watu wote.
*W. Twakuomba utusikie.*
*TUOMBE;*
Ee Yesu Bwana wetu, uliyesema “Pasipo Mimi hamuwezi kitu” umpeleke Roho Mtakatifu atuangaze akili zetu, tupate kufahamu mapenzi yako na kuyatimiza kwa imani na uchaji. Roho Mtakatifu atuongoze katika mambo yote, yeye anayeishi na kutawala nawe pamoja na Baba daima na milele.
*W. Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)*

*NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TISA,*
*JUMAMOSI : ROHO MTAKATIFU ANATUPA MAPENDO*
Maandiko Matakatifu yanatuambia ya kuwa, Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ndiye Upendo katika Baba na Mwana. Upendo hujieneza. Naye Roho Mtakatifu aliye pendo lenyewe la Mungu, hupenda kujieneza na kujishirikisha nasi, na kuwasha ndani yetu moto wa mapendo yake.
Roho Mtakatifu ndiye mwenye kutakatifuza roho zetu kwa neema ya utakaso. Neema hiyo ni uzima wa Mungu, ndio huo upendo wa Mungu tunaoshirikishwa. Roho isiyo na neema ya utakaso imetengana na Mungu, haina uzima wake, haina upendo wake, kwa hiyo haiwezi pia kuwa na mapendo ya kweli ya jirani.
Ingawa tunaona ishara nyingi za watu kupendana kidugu hapa duniani, mapendo hayo si mapendo ya kweli wala si kamili kama hayatokani na neema ya utakaso rohoni mwa mtu. Kama hakuna neema ya utakaso ndani yetu, Mungu pia hayupo kati yetu.
Roho Mtakatifu anatuunganisha na Mungu katika upendo. Pasipo na mapendo hapana mapatano, hapana masikilizano wala mwungano. Watu wanaopendana wanaungana na kulingana katika fikra zao na nia zao. Roho Mtakatifu anayetutia mapendo rohoni na kutuwashia moto wa mapendo, ndiye anayetuwezesha kuwa na mawazo ya namna moja na nia moja.
Watu wanaopendana hupenda kukaa pamoja, kuishi pamoja na kusaidiana. Roho Mtakatifu aliye chanzo cha mapendo ya kweli hutuweka pamoja katika Kanisa lake. Hukaa ndani yetu, hukaa katika Kanisa na kuwasha moto wa mapendo yake ndani yetu. Roho Mtakatifu anatuwezesha kukaa kwa amani nyumbani, kazini na katika jumuiya zetu. Basi, tumwombe sasa Roho Mtakatifu atuongezee hayo mapendo yake ndani yetu.
1) Ewe Roho Mtakatifu, uwashe mioyoni mwetu moto wa mapendo yako, tupate kuwapenda jirani zetu kama tunavyotaka kupendwa nao.
*W. Twakuomba utusikie*

2) Udumishe ndani yetu neema hiyo ya mapendo yako, tuwezeshe kuishi kwa amani leo na siku zote za maisha yetu.
*W. Twakuomba utusikie*
3) Utujalie neema na nguvu za kutekeleza mema yote tunayokusudia kuyatenda siku hii ya leo
*W. Twakuomba utusikie*

4) Uongoze nia zetu na maazimio yetu, yalingane na juhudi zetu za kutaka kuleta mafanikio ya roho na mwili kati yetu,
*W. Twakuomba utusikie*

5) Utubariki, ili baada ya maombi haya, tuwe na juhudi ya kutimiza vema zaidi wajibu wetu wa kikristu kwa moyo mkuu. *W. Twakuomba utusikie*
6) Utuwezeshe kueneza mapendo na amani kati yetu na katika jumuiya zetu za kikristu
*W. Twakuomba utusikie*

7) Utuwezeshe kuwa kweli chachu ya wema na mapendano kati ya watu, ili nao wapate rehema zako kwa maombezi yetu.
*W. Twakuomba utusikie.*
*TUOMBE;*
Ee Mungu, tunakushukuru kwa neema ulizotujalia, hata tukaweza kuifanya ibada hii ya Novena takatifu mpaka mwisho. Utujalie mema yote tuliyoomba; utusaidie kutekeleza yote yale tuliyokusudia kutenda. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
*W. Amina*
*LITANIA YA ROHO MTAKATIFU*
Bwana Utuhurumie………Utuhurumie
Kristu utuhurumie……..….Utuhurumie
Bwana utuhurumie….. Utuhurumie
Baba mweza wa vyote….. Utuhurumie
Yesu Mwana wa Pekee wa Baba na Mwokozi wa Dunia…….Utuokoe
Roho wa Baba na Mwana aunganishaye maisha ndani ya Baba na Mwana………….Ututakatifuze
Roho Mtakatifu……….Utusikie
Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana…………..Njoo ndani ya mioyo yetu
Ahadi ya Mungu Baba……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Mionzi ya Mwanga kutoka Mbinguni……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Mwandishi wa vyote vilivyo vizuri……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Chanzo cha Maji ya Uzima……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Moto utumikao daima……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Muungano Mtakatifu……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
Roho wa ukweli na upendo……………………Utuhurumie
Roho wa hekima na elimu……………………Utuhurumie
Roho wa shauri na nguvu……………………Utuhurumie
Roho wa akili na neema ya kumtumikia Mungu……Utuhurumie
Roho wa neema na sala……………………Utuhurumie
Roho wa amani na subira……………………Utuhurumie
Roho wa usafi na uaminifu……………………Utuhurumie
Kitulizo cha Roho……………………Utuhurumie
Roho aletaye Utakatifu……………………Utuhurumie
Roho uongozaye Kanisa……………………Utuhurumie
Zawadi kutoka kwa Mungu juu Mbinguni……………Utuhurumie
Roho ajazaye ulimwengu……………………Utuhurumie
Roho Mtakatifu…………………..tupe neema ya kuchukia dhambi
Roho Mtakatifu…………….njoo ufanye upya sura ya ulimwengu
Roho Mtakatifu…………………..jaza roho zetu kwa mwanga wako
Roho Mtakatifu……………….ifuraishe mioyo yetu kwa sheria yako
Roho Mtakatifu………………..washa moto wa mapendo ndani yetu
Roho Mtakatifu………jaza mioyo yetu na hazina ya neema yako
Roho Mtakatifu…………………..tufundishe kusali vyema
Roho Mtakatifu…………………..tuangaze kwa nguvu zako za Ki-Mungu zitupatiazo moyo wa kutenda daima yaliyo mema
Roho Mtakatifu…………………..tuongoze Kwenye njia ya wokovu
Roho Mtakatifu……………..tuweze kufahamu yale ya muhimu tu
Roho Mtakatifu……………..tupe hamu ya kuitafuta fadhila yako
Roho Mtakatifu…………………tusaidie tuweze Kupata fadhila zote
Roho Mtakatifu….tupe uvumilivu tuweze kutenda yaliyo mema tu.
Roho Mtakatifu…………..tunaomba uwe zawadi ya uzima wetu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia……….Tushushie Roho wako Mtakatifu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia…………jaza mioyo yetu kwa mapaji yako ya Roho Mtakatifu
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia……….tupe roho ya hekima na neema ya kumsifu Mungu.
Njoo Roho Mtakatifu uzijaze roho za waumini wako uwashe moto wa mapendo yako ndani ya mioyo yetu (W)
*TUOMBE*
Ee Mungu Baba mwenye huruma tujalie Roho wako alete Mwanga kwetu ili apate kututakasa na kuingiza ndani ya mioyo yetu Baraka za kuweza kutenda yale yaliyo mema.
Tunaomba hayo kupitia kwa Mwanao Mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo, anbaye anaishi na kutawala pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu. *AMINA*
*Atukuzwe Baba…..x3*