MATANGAZO:  JUMAPILI KUU YA MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO – 11/06/ 2023

  1. Leo ni Jumapili ya fungu la kumi,kwa wakristo ambao wamejitayarisha na pia wale ambao wametuma fungu lao la kumi  kwa paybill ya kanisa  tunawaalika wajongee mbele kwa maombi na baraka.Tunapokuja mbele tunaombwa kuweka nia zetu pamoja na fungu la kumi tunalomtolea Mungu.Paybill ya kanisa ni 4042525 account Tithe.
  2. Leo, Kanisa linasherehekea Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Kristo (Corpus Christi). Punde tu baada ya Misa hii, kutakuwa na ibada ya kumwabudu Bwana wetu Yesu Kristu, aliye hai katika Sakramenti Takatifu ya Ekaristi.
  3. Wakristo ambao waliacha kupokea  na hawako kwa ndoa na wangependa kurudi kupokea Sakramenti Takatifu, wanaombwa kuona Padre kwa ofisi siku na masaa ya kazi au, wapige simu kujadiliana na Padre siku ingine yeyote wanaweza kupatikana.
  4. Josil Ushindi group watakuwa na siku ya maombi Jumamosi ijayo tarehe 17/06/2023 kuanzia saa tatu asubuhi.
  5. Kikundi cha kina Baba (CMA) wanaalikwa kwa mafundisho yao Jumapili ijaya ya tarehe 18th June 2023 baada ya Misa ya kwanza
  6. Padre kutoka Lodwar atatembelea Parokia yetu Jumapili ijayo tarehe 18th Juni 2023. Kupongeza Wakristo kwa ukarimu ambao tumeonyesha   familia ya Lodwar na pia kuomba msaada ili aweze kuendelea kuhudumia wakristo wa Lodwar.  Wakristo wanakaribishwa kuchukua bahasha ambazo tutamkabidhi mgeni wetu Jumapili ijayo.
  7. Tumeanza usajili wa Watoto wachanga kwa ajili ya ubatizo. Wazazi wanaopenda Watoto wao wachanga wabatizwe wanaombwa kujiandikisha katika Jumuiya zao.

          Jumuiya service

            Jumapili Hii                                                               Jumapili Ijayo

1st Mass: St. Rita                                                      1st Mass: St. Gabriel

2nd Mass: St. Timothy                                              2nd Mass: CWA